Kila msanii ana stori yake, lakini stori ya Vanillah ni ya muhimu. Kutokea Mwanza, alipoanza kucheza na gitaa dogo na kuandika nyimbo kama Utu wa Alikiba, akiwa bado hajatambulika kama msanii, hadi kushinda mashindano ya Super Nyota mwaka 2019, safari yake imejengwa kwa uvumilivu, ujuzi, na ndoto kubwa.
Leo, Vanillah amechaguliwa kwenye programu ya Apple Music Up Next, hatua ambayo ni kubwa sio tu kwa msanii binafsi, bali kwa Bongo Flava nzima. Programu hii inamuweka kwenye mwanga mapema, ikimpa nafasi ya kufikia uwanja wa kimataifa. Huu ni mkakati wa maendeleo ya msaniii kuonekana, kuaminika, na simulizi inayoeleweka kwa msanii anayendelea kukua.
Apple Music inamtambulisha kama msanii “anayesaidia kuboresha aina ya muziki wa Afrika Masharki”, akitengeneza daraja kati ya Bongo Fleva na Afro-pop ambayo inaweza kueleweka kwa mashabiki wa kimataifa.
Kuchaguliwa kwa Vanillah pia ni hatua kubwa kwa ukuaji wake binafsi. Inamuweka mbele ya mashabiki wapya, kumtambulisha kama msanii anaye “boresha muziki” wa East Africa, na kumjengea imani kubwa ndani ya kiwanda cha muziki. Programu hii inafungua milango ya mtandao wa kimataifa, kolabo, na Kuonekana kwenye media, huku ikimsaidia kudumisha udhibiti wa stori yake.




