Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Harmonize, amewapa mashabiki wake zawadi ya kipekee ya Krismasi baada ya kutangaza kuwa ataachia nyimbo tatu kwa siku moja, Desemba 25.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ametaja nyimbo hizo kuwa ni “Leo” akimshirikisha Mbosso, “Sixth Round” akiwa na Yana Toma, pamoja na “Uko Wapi” akiwashirikisha Focalistic na Chicco.
Katika ujumbe wake kwa mashabiki, Harmonize amesema kuwa nyimbo hizo ni zawadi ya Krismasi na amewashukuru mashabiki kwa kuendelea kumuunga mkono, akisisitiza kuwa ni muda wa kusherehekea.
Wimbo wa “Leo” umeonekana kuvutia zaidi kutokana na ushirikiano wa Harmonize na Mbosso, wasanii waliowahi kufanya kazi chini ya lebo moja hapo awali, na sasa wakikutana tena kwenye kolabo inayotarajiwa kuwagusa mashabiki wengi.
Kwa ujumla, Krismasi hii inatarajiwa kuwa ya burudani kubwa kwa mashabiki wa Harmonize, huku nyimbo hizo tatu zikitarajiwa kuleta ladha tofauti kwenye muziki wa Bongo Fleva.
